Jumatano , 21st Feb , 2018

Mbunge wa Ubungo, Mh. Said Kubenea amesema anaungana na wote wenye msimamo wa kumtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Dkt Mwigulu Nchemba ajiuzulu. 

 

Kubenea amesema kwamba Waziri Mwigulu anapaswa kufanya hivyo kwa kuwa hana haiba nzuri ya uongozi kwa kushindwa kutumia vizuri nafasi yake kama Waziri ikiwa ni pamoja na matamshi yake anayoyatoa kuelekeza kwa CHADEMA kuhusika na shambulio lililopelekea kifo cha mwanafunzi wa chuo cha usafoirishaji (NIT).

Katika mkutano wake na wanahabari, Kubenea amesema kwamba moja ya kauli ya mwigulu aliyoitoa ni ile iliyonukuliwa kwenye mtandao mmoja akihoji kwanini ajiuzulu wakati CHADEMA ndiyo wanahusika na mauaji? na kuongeza kwamba tangu waziri huyo alipokuwa Kiongozi wa juu wa CCM hakuwahi kuwa na maadili ya kuizungumzia CHADEMA kwani amekuwa akiihusisha chama hicho na mambo ya kihalifu.

Pamoja na hayo, Kubenea amedai kwamba kama Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni angetoa vibali vya viapo vya Uchaguzi mapema, CHADEMA wasingeandamana na huu uchunguzi ungekua halali haya yote yasingetokea