Linah ambaye amelelewa sana katika maisha ya dini pamoja na kutumika kanisani amesema kwa mara ya kwanza alimuumiza baba yake alipoachana na kuimba kanisani na kujiingiza kwenye nyimbo za kidunia lakini pia hili la kupata mtoto kabla ya ndoa ni jamb lililomuuma zaidi kwa mara ya pili.
Linah amefunguka hayo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa kijamii facebook wa EATV kila Jumatano kuanzia majira ya saa 8:00 mchana hadi 10:00 alasiri.
Hata hivyo Linah amedai kuwa japokuwa baba yake alikasirikia kitendo chake hicho lakini pia amefarijika kuona kwamba amepata mtoto kwani ni muda mrefu alikuwa akiulizwa kuhusu yeye kuolewa na kupata mtoto na kuongeza kwamba angalau sasa hivi wazazi wake wanafarijika kumuona mjukuu wake.
Mbali na hayo, Pamoja na kwamba msanii huyo tayari amepata mtoto amedai kuwa hayupo tayari kufunga ndoa kwa sasa kutokana na kuwepo kwa baadhi ya vitu vinavyowakwamisha kufanya hivyo yeye na mzazi mwenzake.




