Jumamosi , 17th Nov , 2018

Kuelekea uchaguzi mkuu wa Yanga unaotarajiwa kufanyika Januari 13, 2019, wagombea wengine wawili wamejitosa katika nafasi ya Uenyekiti wakiunga na Jonas Tiboroha pamoja na Yono Kevele.

Makao makuu ya Yanga

Kwa mujibu wa ripoti ya kamati ya Uchaguzi ya TFF mabayo ndio inasimamia uchaguzi huo chini ya mwenyekiti wake Malangwe Mchungahela, wagombea hao wawili waliochukua fomu ni Mbaraka Igangula na Titus Osoro.

Kati ya hao, Kevele na Osoro wao wamechukuwa fomu mbili, ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kila mmoja ambapo Kamati ya uchaguzi imesema watatambua fomu moja pekee itakayojazwa na wagombea hao mara watakaporudisha.

Wajumbe waliojitokeza mpaka sasa ni 17 ambao ni Mussa Katabalo, Salim Seif, Benjamini Jackson, Pindu Luloya, Silvester Haule, Hamad Islam na Shaffii Amri.

Wengine ni Said Baraka, Dominic Francis, Ally Msigwa, Leonard Malongo, Salum Chota, Ramadhan Said, Geofrey Mwita, Faustine Mabula, Frank Kalokola na Arafati Haji.