
Kushoto ni Abdukiba, Wastara na Alikiba.
Wastara amefunguka hayo kwenye eNewz akisisitiza kuwa hana ukaribu na wasanii hao kama zamani kutokana na Team Kiba kumtukana sana kipindi ambacho kijana mmoja anayesemekana kuwa wa karibu na familia ya Alikiba kukamatwa akiwa kwake.
''Sijawahi kutoka kimapenzi na Alikiba au Abdukiba walikuwa marafiki zangu na wadogo zangu tu lakini nilivunjika moyo kuwapost mitandaoni kutokana na Team zao kunitukana sana kwa jambo ambalo hata sikuhusika'', ameeleza.
Mwigizaji huyo pia amesisitiza kuwa familia ya Alikiba ni watu wake wa karibu sana lakini ushirikiano wa mitandaoni aliacha tangu yalipomkuta matatizo hayo.
Alikiba nampenda na kama familia yangu na itabaki hivyo maana siwezi tena kumpost mitandaoni kama nilivyokuwa nafanya zamani nikijisikia tu kwasasa ni ngumu kutokana na yaliyotokea.