Jumanne , 25th Dec , 2018

Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mwita Waitara ameitaka Wakala wa Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (DART) kuangalia namna ya kuboresha utendaji, ili kuhakikisha mradi huo unaweza kutumika kwenye utekelezaji wa miradi mingine ya serikali.

Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mwita Waitara.

Waitara ametoa agizo hilo alipotembelea mradi huo jana na kuona tiketi za abiria zikichanwa badala ya kuingizwa katika mashine kama ilivyokuwa awali jambo ambalo amesema linampa hofu kuwa huenda kuna upigaji unaweza kufanyika.

Serikali imewekeza fedha nyingi katika mradi huu kila mmoja ana fahamu, tunataka kila senti hapa ilipiwe kodi na kila kiasi kinachokusanywa kifahamike lakini mashine zikiwa hazifanyi kazi kama hivi napata wasiwasi wa upigaji,” alisema Waitara.

Mradi wa mabasi yaendayo haraka nchini umekuwa ukiingia kwenye mgogoro wa mara kwa mara juu namna ya uendeshaji, ambapo abiria mbalimbali wamekuwa wakilalamika juu ya utoaji wa huduma hiyo.