Jumatatu , 18th Mar , 2019

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dkt Vincent Mashinji amempongeza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF kwa hatua yake ya kujiunga na Chama cha ACT- Wazalendo na kusema uamuzi wake ni sahihi.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dkt Vincent Mashinji.

Katibu Mkuu wa CHADEMA Vincent Mashinji ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na www.eatv.tv iliyotaka kufahamu juu ya maoni yake kama kiongozi wa juu wa chama kikuu cha upinzani nchini.

Mashinji amesema, "nimpongeze kwa uamuzi wake wa kuendelea na shughuli za kisiasa na kupigania mabadiliko kwenye taifa letu, watu wengi walitegemea yeye kupumzika lakini amejipima na ameona anahitaji kuendelea kufanya kazi ni hatua kubwa kwetu sisi wapinzani."

Mapema leo Machi 18, 2019 Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam, ilitangaza kutambua uhalali wa mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Profesa Ibrahim Lipumba.

Kufuatia maamuzi hayo ya Mahakama majira ya saa nane leo Machi 18, 2019 alitangaza uamuzi wa kuhamia Chama Cha ACT- Wazalendo kwa kile alichokidai amesoma katiba za vyama vingine na kubaini masharti ya chama hicho ni nafuu zaidi.