Hayo ameyabainisha wakati akizungumza na wafanyabishara pamoja na Mabalozi wanaowakilisha nchi ya Tanzania katika mataifa ya Kenya, Rwanda, Burundi na DR Congo katika kongamano la wiki ya uwekezaji mkoani humo.
"Mwaka 2010 pato la mwananchi wa Kagera lilikuwa takribani Tsh, 667,000, toka mwaka 2018 kwa takwimu zilizopo pato la mwananchi wa Kagera ni Tsh, 1300, 000 lakini pato jumla la mkoa limepanda toka Tsh, 1.3 trilioni mwaka 2010, mpaka Tsh, 4.9 trilioni mwaka 2018", amesema RC Gaguti.
Aidha RC Gaguti ameongeza kuwa Kagera ni mkoa wa 24 kati ya mikoa 26, ambao unachangia asilimia 3.6% katika pato la Taifa.