Jumanne , 17th Dec , 2019

Mvua zilizoanza kunyesha leo asubuhi ya Disemba 17, 2019, jijini Dar es salaam, zimepeleeka mafuriko katika baadhi ya maeneo ya jiji hilo na kusababisha kadhia na kero mbalimbali kwa wananchi.

Mvua jijini Dar es salaam.

EATV imetembelea katika baadhi ya maeneo ya Jiji hilo ikiwemo Tandale kwa Ali Maua, ambapo ilishuhudia vitu mbalimbali vikisombwa na maji hayo ikiwemo Sofa.

Akizungumza na baadhi ya wananchi wa eneo hilo Mtangazaji wa EATV, Samson Charles, wamesema kuwa "hali hiyo imekuwa ikijirudia mara kwa mara na kuiomba Serikali kuingilia kati"

Aidha katika mafuriko ilishuhudia moja ya watu wakijitolea kuwaokoa watoto kwa kuwavusha kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

Ambapo pia Mvua hiyo imetajwa kuathiri maeneo mengine ikiwemo Magomeni, Shekilango, Sinza na andale.

Tazama hapo chini.