Jumatatu , 23rd Dec , 2019

Mkuu wa mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali Nicodemas Mwangela ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumshikilia mkandarasi anaesambaza vifaa vya ujenzi katika Soko Kuu la Mazao la Kakozi Wilaya ya Momba.

Mkuu wa mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali Nicodemas Mwangela

Brigedia Jenerali Mwangela ameitaja kampuni hiyo kuwa ni NUI COMPANY LTD, ambapo mkandarasi huyo ameshikiliwa mpaka atakapopeleka vifaa vyote vinavyohitajika eneo la ujenzi.

Akizungumza leo Disemba 23, mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa mkandarasi anashikiliwa kwa siku ya tatu sasa kwa sharti la kupeleka vifaa vinavyohitajika au kulipa fedha zilizobakia kukamilisha mradi huo ili aweze kuachiwa.

Amesema mkandarasi ameshaanza kusambaza vifaa lakini kwa kusuasua, hivyo atakapokamilisha ndipo ataachiwa huru.

Mtazame Mkuu wa Mkoa  akizungumza.