
Mchezo wa Simba na Azam FC
#FAHAMU Nusu Fainali ya pili ya Kombe la Mapinduzi inachezwa leo kati ya @azamfc na @SimbaSCTanzania baada ya Mtibwa Sugar kutangulia fainali kwa kuiondoa Yanga kwenye mikwaju ya penalti.
Azam FC Vs Simba SC - saa 2:15 Usiku pic.twitter.com/ot9jnqNl0Y
— East Africa TV (@eastafricatv) January 10, 2020
Mchezo wa leo ni wa tano kuzikutanisha Azam FC na Simba katika michuano ya Mapinduzi ndani ya miaka saba ya karibuni, ambapo mara zote Azam FC imeibuka na ushindi kwa kuiondoa Simba. Mchezo wa kwanza Januari 2012, Azam iliichapa Simba katika Nusu Fainali kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Kipre Tcheche na John Bocco.
Mchezo wa pili uliochezwa mwaka 2016, Azam FC ilikutana na Simba katika Nusu Fainali na kutoka sare ya mabao 2-2 na kisha Azam FC kwenda fainali kwenye mikwaju ya penalti. Mwaka 2017 Azam FC iliifunga Simba bao 1-0 katika fainali na mwaka 2019 pia Simba ikafungwa mabao 2-1 katika Nusu Fainali.
Katika miaka hiyo minne iliyokutana na Simba, Azam FC imefanikiwa kubeba ubingwa mara zote nne. Je, Simba itakubali kuwa mteja wa Azam FC kwa mara ya tano au itapindua meza hii leo?.