Rais Magufuli
Rais Magufuli amesema hayo wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa nyumba 12 za Askari Magereza kwenye Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam, ambapo ameeleza kulikuwa na mkataba ambao ni wa ajabu.
Rais Magufuli amesema kuwa "ninajua Waziri wa Mambo ya Ndani hayupo hapa ameshaandika barua ya kujiuzulu na mimi nimeshamkubalia"
BREAKING NEWS : WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AJIUZULU
Rais Magufuli amethibitisha kuwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amejiuzulu nafasi yake.
"Ninajua Waziri wa Mambo ya Ndani hayupo hapa ameshaandika barua ya kujiuzulu na mimi nimeshamkubalia" - @MagufuliJP pic.twitter.com/Qap07Koc2G
— East Africa TV (@eastafricatv) January 23, 2020
"Palikuwa na mkataba wa ajabu unatengenezwa mambo ya ndani, wa zaidi ya Tril. 1 na umesainiwa na Kamishna wa Fire,na haujapangwa na kupitishwa na Bunge, wakati wa vikao na kampuni moja walipokuwa wakienda kwenye mkutano walilipana pesa nyingi" ameongeza Rais Magufuli