Picha ya MwanaHipHop Stamina
Akiiambia Planet Bongo ya East Africa Radio, inayoruka kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 7:00 mchana mpaka 10:00 jioni, Stamina amesema zamani alikuwa anafanya hivyo bila ya kujua thamani ya mwanamke.
"Mimi nimeshawahi kufumaniwa hapo zamani sijawahi kuwa muaminifu, nilikuwa na mwanamke mmoja ambaye nilimtesa kidogo kwa sababu sikuwa na mipango naye ila kumbe yeye alikuwa yupo serious kwangu, tena nilifumaniwa mara 2 na mwanamke huyohuyo mmoja wakati huo nilikuwa sijatulia, sijui nilikuwa sioni thamani yake" amesema Stamina.
Stamina ni moja ya wasanii ambao walikuwa gumzo wiki kadhaa zilizopita, baada ya kuachia wimbo wake wa asiwaze, ambapo amezungumzia yaliyomtokea kwenye ndoa na alivyosalitiwa na mke wake, hali iliyopelekea kuachana kwao.