Jumatano , 10th Jun , 2020

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. Magufuli leo Juni 10, 2020 ameongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika Chamwino mkoani Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 10 Juni 2020.

Katika kikao hicho wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo kupitia Ilani ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa 2020 unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Kamati imepitia kwa mara pili Ilani hiyo na kuelekeza maandalizi ya mwisho ili Ilani iwasilishwe Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu kwa uamuzi wa mwisho.

Soma taarifa kamili hapo chini