Upande wa kushoto ni msanii Snura, kuli ni Shilole
Akifunguka kuhusu hilo kupitia EATV & EA Radio Digital, Snura amesema hana kinyongo na mtu yeyote na kilichotokea amechukulia kama changamoto japo imemuumiza.
"Nimekaa kimya na kumuachia Mungu maana itakuwa kama nongwa kuliendeleza ikiwa kama watoto wa kike kuongea masuala ya ugomvi muda wote, sina kinyongo na mtu yeyote kilichotokea ni changamoto katika maisha, namuachia mungu maana hakuna shari isiyo na kheri kwa hiyo nikiwekea kinyongo Mungu ananiondolea vizuri na baraka ambazo nilitakiwa nipate, wakati mwingine changamoto inaumiza lakini inakuwa haikukatishi tamaa" amesema Snura
Shilole alimchana Snura mbele za watu kwenye tamasha la Girl Power baada ya kupigwa na Uchebe kwa kusema hakupendezwa na kauli za Snura baada ya kutokea kwa tukio hilo.