Jumatano , 19th Aug , 2020

FC Barcelona imemtangaza aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi Ronald Koeman kuwa kocha mpya wa kikosi hicho kwa mkatab wa miaka miwili utakao malizika juni 30 mwaka 2022.

Kocha mpya wa FC Barcelona Ronald Koeman

Raia huyo wa Uholanzi anachukua nafasi ya kocha Quique Setien aliyefutwa kazi siku ya jumatatu agost 17 2020 baada ya timu hiyo kuondolewa kwenye michuano ya klabu bingwa ulaya Uefa Champions League kwa kipigo cha aibu cha mabao 8-2 katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Bayern Munich.

Koeman aliwahi kufanya kazi FC Barcelona kama mchezaji kati ya mwaka 1989 hadi 1995 ambapo alishinda matajai manne ya ligi kuu Hisapnia La Liga na ubingwa wa ulaya lakini pia alifanya kazi kama kocha msaidizi chini ya kocha Louis van Gaal kati ya mwaka 1998 hadi 2000.

Kikosi hicho cha mabingwa wa ulaya mara tano pia kimemtangaza Ramon Planes kuwa mkurugenzi mpya wa ufundi wa timu hiyo akichukua nafasi ya Eric Abidal.