
Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu.
Amesema hayo hii leo Agosti 29, 2020, wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho kwa Jimbo la Kawe, ambapo amesema, chochote kilichopo kwenye ilani kinabeba msingi wa kauli mbiu hizo..
"Ilani yetu ya Uchaguzi Mkuu huu ina kauli mbiu yenye maneno yafuatayo, Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu, chochote ambacho tumekisema katika ilani hii msingi wake ni uhuru wa watu msingi wa watu na maendeleo ya watu", amesema Lissu.
Aidha Tundu Lisuu amesema kuwa maendeleo wanayaoyataka yatazingatia uhuru, haki na maendeleo ya Watanzania kama yale aliyoyaita Baba wa Taifa maendeleo ya watu.
"Maendeleo tunayoyataka ni yanayozingatia uhuru wa watu, yanayozingatia haki zao, maendeleo aliyoyaita Baba wa Taifa maendeleo ya watu badala ya vitu", ameongeza.