Msanii Hamis maarufu kama Hamis wa BSS
Akifunguka hilo kwenye show ya Friday Night Live ya East Africa Tv, Hamis BSS amesema si kweli kwamba alihitaji pesa nyingi ili kujiunga Konde Gang, pia amefurahi kuona wasanii wengine walivyotambulishwa Konde Gang bila ya hata yeye kuwepo.
"Si kweli kwamba nilihitaji pesa nyingi kujiunga na Konde Gang, ila ni riziki tu Mungu anatoa kwa kila mtu, mimi kiukweli nimefurahi kwa wasanii waliotambulishwa, Naamini Mungu tu anafanikisha kwa kila mtu kwa wakati wake ila kwa kawaida natamani ningekuwa mimi" amesema Hamis wa BSS