Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo.
Jafo amesema hayo leo, Septemba, 19,2020, wakati anahutubia katika Mahafali ya Kimataifa ya wahitimu waliosoma nje yaliyofanyika Mlimani City Jijini, Dar es salaam, ameahidi kuwapigia debe vijana hao na kuhakikisha katika nafasi walizotoa wanashughulikiwa.
"Nikuhakikishieni tutajitahidi kwa kadri tutakavyotangaza nafasi za ajira, wasomi waliosoma nje kwa ada za wazazi waliohangaika lazima watapata kipaumbele" amesema Waziri Jafo.
Aidha Jafo ameusifu utaratibu wa kuwapeleka vijana kwenda kusoma nje kuwa ni utaratibu utaokasaidia nchi kupanda kiuchumi, "Kwa utaratibu huu kama tukijipanga vizuri kwa pamoja serikali na sekta binafsi kwa pamoja yale malengo ya nchi yetu kuzidi kupaa kiuchumi yatafikiwa".