Jumanne , 22nd Sep , 2020

Serikali ya Uingereza Imesitisha urejeo wa mashabiki viwanjani siku hizi za karibuni kutokana na tishio la maambukizi mapya ya virusi vya Corona.

Mtendaji mkuu wa Manchester United, Ed Woodward ambaye Klabu yake inapoteza Bilioni 12 za kitanzania kila mechi isiyohudhuriwa na mashabiki.

Waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson anatatarajia kulihutubia Bunge la nchi hiyo kuhusiana na mpango huo.

Kumetolewa maoni kutoka kwa taasisi na watu tofauti tofauti, kuhusiana na mpango husika.

Nchi nyingi duniani zilisitisha shughuli mbali mbali zikiwemo za michezo kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na Virusi aina ya Covid-19.

Zilitoka taarifa awali kuhusiana na uwezekano wa mashabiki kuruhusiwa kuingia viwanjani kwa idadi ya namba maalumu kwenye michezo mbali mbali.

 

Lengo lilikua ni kuzingatia angalizo la wataalamu wa afya juu ya njia za kudhibiti maambukizi mapya ya ugonjwa huo.

 

Uingereza ni moja ya nchi ambazo ziliathiriwa kwa kisia kikubwa na homa ya mapafu ambayo ilisababisha vifo vya watu wengi duniani.

Mnamo mwezi wa kumi ilitizamiwa kua ni siku ambayo wapenda michezo wangeanza kuhudhuria viwanjani kwa idadi maalumu, kwa kuzingatia kanuni za kupeana umbalia wa mita mbili kutoka mtu mmoja na mwengine kama ilivyo shauriwa.

 

Michezo mingi Imekua ikichezwa bila mashabiki tangu mwezi wa tatu mwaka kuu kutokana na Covid-19.

Akizungumza mtendaji mkuu huyo wa shughuli mbali mbali za kila siku katika serikali alisema Boris Johnson.”Kurudi kwa mashabiki viwanjani katika michezo mbali mbali haitokua tena tarehe 1 Oktoba , Mawaziri wanahangaika kutafuta njia za kuvisaidia vilabu vya michezo vilivyoathiriwa na mkatazo huo” Boris Johnson.

Kevin Miles,mtendaji mkuu wa wa umoja wa mashabiki wa mpira wa alisema. “Umoja wa mashabiki wa mpira wa miguu , uliandika barua kwa serikali kutilia mkazo juu ya umuhimu wa kuruhusu mashabiki kurudi viwanjani.

 

Mrejesho wa vipimo vya mashabiki kuhusiana na kufata njia zilizowekwa kudhibiti kusambaa kwa Covid-19, vimeonyesha mashabiki walikua wapo salama zaidi viwanjani kuliko kwenye matukio mengine ya kijamii.

Uwepo wa mashabiki kwenye michezo si muhimu tu kwa maisha yao, bali ni muhimu kwa afya ya vilabu ambavyo vina mchango wa moja kwa moja katika jamii.

Mjumuisho wa mapato yanayotokana na viingilio viwanjani na msaada wa serikali unahitajika kuzisaidia timu kujieandesha. Uongozi unapaswa kuwasikiliza mashabiki na timu katika hili.

HASARA ZA KUKOSEKANA MASHABIKI VIWANJANI

KIUCHUMI:
Timu zimepoteza kiasi kikubwa cha pesa kutokana na mashabiki kutokuingia viwanjani, kwa kiasi kikubwa mapato yanapatikana kutokana na viingilio huwa ni chanzo cha kwanza kikubwa cha fedha na husaidia vilabu kujiendesha katika shughuli mbali mbali kama kulipa mishahara na matumizi mengine.

Klabu ya Manchester United, inapoteza kiasi cha pauni milioni 4 ambayo ni sawa na bilioni 12 za Kitanzania katika kila mechi ambayo mashabiki hawaingii kiwanjani.

Uwanja wa nyumbani wa mashetani wekundu Old Trafford unaingiza mashabiki zaidi ya 75000.

HAMASA KWA WACHEZAJI:

Timu zimejikuta zikiwa katika michezo ya nyumbani kama zipo ugenini , hivyo kutengeneza kujiamini kwa timu za ugenini mshabiki huwa ni mchezaji wa kumi na mbili kwa kushangilia huwa kunaongoza hamasa kwa wachezaji na huwachanganya timu pinzani.