
Barabara ya Mkwajuni ikiwa imejaa maji
Wakizungumza na EATV, wakazi hao wamesema kuwa hali sio shwari kwani hali hiyo imekuwa ikijirudia tangu miaka ya 1980, hivyo kuiomba serikali kumaliza kero hiyo.
Kwa upande wao madereva wameeleza kuwa, hali hiyo inapelekea uharibifu wa vyombo vya moto wanavyoendesha lakini wakati mwingine kuhatarisha hata maisha yao kutokana na hatari ya kuvuka maji hayo.
“Ninapopita hapo kuna mawili, nipite salama au chombo changu kizimike katikati ya maji, tunaomba watusaidie kumaliza hii kero” amesema mmoja wa madereva.