Jumatano , 14th Oct , 2020

Wananchi wa mtaa wa Mzambarauni na Machimbo huko Yombo wamelazimika kuweka matuta ya udongo katika barabara ya ndege kwa kile walichoeleza kwamba ni ajali za mara kwa mara ambazo zinasababisha vifo kwa watumiaji wa barabara.

Pichani tuta la udongo lililowekwa na wananchi kuzuia ajali.

Wakiongea leo na Kurasa wananchi hao wamesema kwa siku wanagongwa watu wasiopungua watatu na wengine wanapoteza maisha.

Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Yombo Rahim Maridadi, amesema ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko ya wananchi hao mara kwa mara na kuyafikisha kwa wahusika lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.