
Tyson Furry(kulia), akimsukumia konde Deontay Wilder (kushoto) katika moja ya pigano lao.
Frank Warren ambaye ni promota wa Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 32 amesema kwamba Fury amefutilia mbali mpango wa kuchapana na Deontay Wilder wa Amerika kwa mara ya tatu mnamo Disemba 2020 na tayari amepata mshindani mpya.
Fury aliyemchapa Wilder kwa njia ya ‘Knock-Out’ katika raundi ya saba ya masumbwi yaliyoandaliwa jijini Las Vegas, Amerika mnamo Februari 2020.
Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Fury kumzidi maarifa Wilder baada ya wawili hao kuambulia sare mnamo 2018 jijini Los Angeles, Amerika.
“Natamani sana kurejea ulingoni kuendelea kufanya kitu ninachokifahamu vyema zaidi,” alisema Fury.
Fury amesema: “Nawahakikishia mashabiki wangu kwamba nitakuwa ulingoni mnamo Disemba 5 jijini London. Mpinzani wangu atajulikana chini ya kipindi cha wiki moja ijayo. Tarajieni mambo makubwa.”
Fury hajawahi kushiriki mashindano yoyote nchini Uingereza tangu Agosti 2018 na mashindano yake manne yaliyopita yaliandaliwa nchini Amerika.
“Pigano langu dhidi ya Wilder lilikuwa awali lifanyike Julai 2020 kabla ya kuahirishwa hadi Oktoba kisha Disemba 19.
Sasa waandalizi wamezungumzia uwezekano wa pambao hilo kufanyika mwaka ujao wa 2021 japo nimechoka sana kusubiri na huenda nikateua kususia,” alisema Fury.