
Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi
Akizungumza mara baada ya ziara, Dkt.Mwinyi, ameweka wazi kuwa ujio wake katika hospitali hiyo umetokana na taarifa kutoka kwa baadhi ya wagonjwa wanaofika kwenye hospitali hiyo ambao wanalalamika juu ya kutokuridhishwa na huduma zinazotolewa hospitalini hapo.
“Nimeangalia wauguzi, nimeangalia madaktari hakuna aliyevaa jina ili atambulike hiyo ni kasoro kubwa katika utoaji wa huduma ya afya, kwanza lazima mtu atambulike kama anatoa huduma ili kama mtu ana tatizo aseme hakufanyiwa huduma nzuri na nani kwa hili nitawataka uongozi warekibishe mara moja” amesema Dkt.Mwinyi
“Nimeona kuna baadhi ya huduma hazifanyika si kwa sababu hatuna fedha ni tatizo la kiutendaji na kuna matatizo madogomadogo ambayo kama yangeshughulikiwa huduma zote zingekuwa bora, kuna uhaba wa dawa, mashuka na vifaa kuna uhaba kila sehemu na hakuna sababu za kifedha” ameongeza Dkt.Mwinyi
Aidha Dkt.Mwinyi ametoa muda wa miezi mitatu kwa hospitali hiyo kuhakikisha inaboresha huduma zake ili kuondoa kero wanazokumbana nazo wagonjwa wanaofika kwa ajili ya matibabu.