Pichani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Hukumu hiyo imetolewa hii leo na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Jijini Dar es salaam.
Awali, akisomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Godfrey Ngwijo, alidai, Novemba 24, mwaka huu mshtakiwa alibainika na makosa mawili ambayo ni kuingia nchini bila kibali na baada ya hapo aliishi bila kibari eneo la Ubongo jijini Dar-es-Salaam.
"Nimekiri makosa kwa sababu naipenda Tanzania na kuna ndugu zangu wako hapa na nampenda Rais John Pombe Magufuli kwa sababu kaikomesha corona" amesema mshtakiwa
Hata hivyo Mshtakiwa amefanikiwa kulipa faini yote na kuepuka kifungo cha mwaka mmoja.