Jumatano , 2nd Dec , 2020

Mick Schumacher, mtoto wa bingwa mara saba wa ulimwengu wa mashindano ya Langalanga,Michael Scumacker amesaini kmkataba wa kuitumikia timu ya Haas msimu ujao.

Mick Schumacher akishangilia ushindi.

Timu hiyo yenye makao yake nchini Amerika ilisema kijana huyo wa miaka 21 alikuwa amesaini mkataba wa miaka mingi na atashirikiana na Mrusi Nikita Mazepin, ambaye alithibitishwa Jumanne.

Schumacher, mshiriki wa Chuo cha udereva cha Ferrari, anaongoza safu ya langalanga daraja la pili kwenda kwenye raundi ya mwisho ya wikendi hii.

Iwapo ataingia katika mashindano ya langalanga daraja la kwanza mwakani,itakuwa anaadhimisha pia kwenye kumbukumbu ya miaka 30 ya baba yake mwenyewe kuingia kwenye mchezo huo, kwenye Grand Prix ya Ubelgiji ya 1991.