
Kushoto ni picha ya Shilole na Rommy enzi hizo na kulia ni Shilole kwa sasa
Rommy mwenyewe amethibitisha hilo ikiwa leo Disemba 20, 2020 ikiwa ni siku ya kuzaliwa ya Shilole, ambapo ameeleza kuwa waliwahi kuwa na mahusiano huko nyuma kisha wakaachana.
''Nichukue nafasi hii ya siku yako ya kuzaliwa Shilole kukwambia kua Nakupenda Sana Darling na nashukuru Mungu kwa kutukutanisha tena kwenye maisha yetu ikiwa kila mmoja wetu ameshatimiza malengo yake'', ni sehemu ya ujumbe wa Rommy kwa Shilole.
Rommy amesema penzi lao limerejea, baada ya ndoa zao wote kuvunjika hivi karibuni na walipokutana wakaongea na kurejesha mapenzi yao.