
Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer.
'The Telegraph' limeeleza kuwa sababu ya uongozi wa klabu hiyo kuamua kuataka kumpa mkataba mpya kocha huyo ni kutokana na imani juu ya kocha huyo baada ya kuijenga timu hiyo kwa kiasi kikubwa.
Baada ya kutolewa na Leicester City kwenye hatua ya robo fainali ya kombe la FA la nchini England, sasa Manchester United imesalia kwenye michuano ya UEFA EUROPA hatua ya robo fainali baada ya kuindoa AC Milan ya Italia.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, hata kama Solskjaer atashindwa kutwaa taji hilo na kutoka kapa msimu huu basi kocha huyo bado ataendelea kuwa kocha wa kikosi hicho kinachoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa EPL akiwa na alama 57 utofauti wa alama 14 na kinara Manchester City.
Solskjaer amesalisha kanadarasi ya mwaka mmoja na mashetani hao wekundu hadi mwaka 2022.