Jumatatu , 31st Mei , 2021

Rasimi klabu ya FC Barcelona imekamilisha usajili wa mshambuliaji Sergio Kun Aguero kutoka Manchester City.

Sergio Kun Aguero

Barcelona na Aguero wamefikia makubaliano ya mchezaji huyo kujiunga na klabu hiyo kwa mkataba utakao anza Julai 1, 2021 na kumalizika msimu wa 2022-23, anajiunga na timu hiyo akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na   Manchester City kumalizika Juni 30 2021.

Katika mkataba wake na Barcelona kimewekwa kipingele cha timu itakayomuhitaji mchezaji huyo pindi akiwa kwenye mkataba itapaswa kulipa ada ya uhamisho ya Euro million 100 ambayo ni zaidi ya bilioni 282 kwa pesa za kitanznaia.

Aguero raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 32, anaondoka Manchester City baada ya kuitumikia kwa misimu 11, alijiunga na timu hiyo mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid ya Hispania.

Kun anaondoka City akiwa mfungaji bora wa muda wote akiwa na mabao 260 lakini pia ndio mchezaji aliyeshinda mataji mengi kwenye historia ya klabu hiyo, ametwaa jumla ya mataji 15 akiwa na timu hiyo kutoka jiji la Manchester.