Jumatano , 2nd Jun , 2021

Wakali na waliokuwa vinara wa ukanda wa mashariki kwenye ligi ya kikapu nchini Marekani, Philadelphia 76ers itakuwa timu ya tamu kufuzu hatua ya nusu fainali kwenye michezo ya mtoano ya ligi hiyo endapo watafanikiwa kuifunga Washington Wizards saa 8:00 usiku wa kumkia kesho.

Nyota wa Clippers, Kawhi Leonard akimpita mlinzi wa Dallas Mavericks kwenye mchezo wa NBA Playoff game 4.

Philadelphia 76ers wanaongoza kwenye michezo yake 3 hivyo wakipata ushindi watafikisha ushindi kwenye michezo 4 ikiwa ni ushindi wa michezo mingi zaidi ya Wizards wenye mmoja na hawatoweza kufikia ushindi wa michezo minne.

New York Knicks watakipiga na Atalanta Hawks saa 8:30 usiku wa kuamkia kesho kwenye dimba la Madison Square Garden nchini Marekani huku Atalanta na yeye akisaka ushindi tu ili kufuzu nusu fainali ya ligi hiyo.

Waliokuwa vinara na ambao ni wakali wa ukanda wa Magharibi, Utah Jazz wataungurumishana na Memphis Glizzles saa 10:30 Alfajiri ya kuamkia kesho kwenye dimba la Vivint Smart Home nchini Marekani wakihaha kusaka ushindi mmoja kufuzu nusu fainali ya NBA.

Dallas Mavericks ambao wanatoka jasho juu ya utimamu wa nyota wake Luka Doncic mweney maumivu ya goti, watajitupa dimbani saa 11:00 alfajiri ya kuamkia kesho kukipiga na ugenini na Los Angeles Clippers kwenye uwanja wa Staples Center wawili hao wakiwa na sare ya michezo 2.