Wachezaji wa Denmark wakishangilia bao kwenye mchezo dhidi ya Urusi
Denmark ilipoteza miwchezo miwili ya kwanza ya kundi B, dhidi ya Finland kwa bao 1-0, wakafungwa na Ubeligiji mchezo wa pili kwa mabao 2-1, kabla ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Urusi kwenye mchezo wa mwisho jana usiku na ushindi huo umewafanya wafuzu hatua ya 16 bora na imekuwa timu ya kwanza kufanya hivyo.
Alama tatu walizopata kwenye mchezo dhidi ya Urusi zimewafanya wamalize nafasi ya pili kwa faida ya magoli ya kufunga na kufungwa licha ya kuwa na alama sawa na Finland na Urusi wakati timu ya taifa ya Ubeligi wamemaliza wakiwa vinara wa kundi wakiwa na alama tisa, baada ya kushinda michezo yote.
Na sasa Denmark watacheza dhidi ya Wales kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora, mchezo utakao chezwa Juni 26 kwenye uwanja wa Johan Cruyff huko Amsterdam Uholanzi.






