Jumatatu , 5th Jul , 2021

Mshindi wa tuzo ya Grammy na BET, Burna Boy kutoka nchini Nigeria ameweka wazi kuwa ataachia album yake mpya mwezi Agosti 14 wakati album yake ya “Twice as Tall” ikiwa inatimiza mwaka mmoja tangu itoke.

Picha ya Msanii Burna Boy

Album hiyo ijayo itakuwa ni ya 6, huku ikilezwa kuwa Sean Love Combs (P. Diddy) atakuwa ndiye mtayarishaji mkuu (executive producer)  wa album hiyo ikiwa ni kwa mara ya pili baada ya kufanya hivyo kwenye “Twice as Tall”.