
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Rais Samia ametoa kauli hiyo hii leo Agosti 25, 2021, wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Mafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi, Makamanda na Vikosi, na kusema kwamba kuwataka kutenda yaliyo haki.
"Mshutumiwa anapokufa mikononi kwako, Askari wa Polisi umemchukua huko umeshamchapa virungu vya kutosha binadamu sisi tuko wa afya za tofauti tofauti, mwingine hata uchape vipi bado yuko ngangari kmwingine vifimbo viwili tu tayari keshafiki mbele ya haki, kesi za watu kufa kwenye Vituo vya Polisi havileti sifa nzuri," amesema Rais Samia.