
Aliyekuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, William Tate Ole Nasha
Akizungumza kwa niaba ya Rais Samia, Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, ametoa pole kwa familia pamoja na kwa Rais Samia kwa kumpoteza Naibu Waziri mchapakazi na aliyefanya kazi yake kwa uzalendo mkubwa.
Ole Nasha alifariki dunia Septemba 27, 2021 akiwa nyumbani kwake mtaa wa Medeli jijini Dodoma na mwili wake unatarajia kusafirishwa kesho Ijumaa Oktoba Mosi, 2021 kwenda Ngorongoro na mazishi yatafanyika Jumamosi Oktoba 2 mwaka huu.