Picha ya mwandishi wa vitabu Abdulrazak Gurnah
Tuzo hiyo inamfanya kuwa Mwafrika wa pili kushinda na imetangazwa mapema wiki hii na Mats Malm ambaye ni katibu wa kudumu wa Swedish Academy na katika uandishi wake unatajwa kuchochea mabadiliko makubwa kwenye Jamii ikiwemo kuelezea athari za ukoloni na hatima ya wakimbizi.
Gurnah ameandika riwaya takribani 10 kama 'Memory of Departure', ‘The Last Gift’, 'Paradise' na kadhalika huku Tuzo ikiambatana na medali ya dhahabu na fedha taslimu dola Milioni 1.14 ambazo ni zaidi ya Tshs. Bilioni 2.62.