Jumamosi , 9th Oct , 2021

Spika wa Bunge Job Ndugai, amemteua Mbunge wa Kigamboni Dkt. Faustine Ndugulile, kuwa Mjumbe wa Kamati ya Sheria Ndogo na Kamati ya Masuala ya UKIMWI.

Mbunge wa Kigamboni Dkt. Faustine Ndugulile

Mabadiliko hayo madogo yamefanya leo Oktoba 9, 2021, ya Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge kwa kuzingatia matakwa ya kanuni za kudumu za Bunge, ambapo pia amemhamisha Mbunge Humphrey Polepole kutoka kamati ya utawala na serikali za mitaa na kupelekwa kamati ya sheria ndogo.

Wengine waliohamishwa ni Dkt. Godwin Kunambi, aliyehamishwa kutoka Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, na kupelekwa kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii.