Jumatano , 10th Nov , 2021

Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge, ametoa siku 21 kwa wilaya zote za mkoa huo kwamba wawe wamekamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 881, ili kuondoa tatizo la watoto kubanana madarasani na kuwezesha kupokea wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge

Agizo hilo limeanza kutelezwa kuanzia Novemba 09 mwaka huu hadi Novemba 30, ambapo kila wilaya itapaswa kuwa imekamilisha idadi ya vyumba vya madarasa wanavyopaswa kujenga.

Akizungumza katika kikao cha maelekezo kilichohudhuriwa na baadhi ya wakurugenzi, maafisa elimu sekondari, wakuu wa shule na wadau wengine, mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasssan, ametoa zaidi ya shilingi bilioni 20 kwa mkoa wa Kagera, kwa ajili ya kujenga vyumba vya madarasa, hivyo hayuko tayari kusikia kuna uzembe katika ujenzi huo.