Jumamosi , 11th Dec , 2021

Watu wanane wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Kagera, kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwanamke aitwaye Stella Paschael mkazi wa Nyabihonza wilaya ya Karagwe, kwa kumkata mapanga na kutoweka na baadhi ya viungo vyake vikiwamo ubongo, ulimi na koromeo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, Awadhi Haji

Kamanda wa polisi mkoani Kagera Awadhi Haji, amesema kuwa mauaji hayo yalitokea Desemba 03 mwaka huu, na wote wamekiri kuhusika na mauaji hayo kwa madai ya kwamba marehemu aliwaua ndugu zao kwa njia za kishirikina.

Amesema kuwa baada ya mahojiano ya kina watu hao walisema walimuua mama huyo kwa sababu kuna vifo vya watu wawili vilitokea katika familia zao, na walipokwenda kwa mganga wa kienyeji waliambiwa kuwa Stella ndiye anahusika na vifo hivyo, na kisha kuweka mipango ya kumuua.