(Marehemu Msanifu Kondo enzi za Uhai wake,)
Taarifa ya kifo cha Kondo, imethibitishwa na Baba yake Mzazi, Bin Kondo ambaye amesema Kondo alisumbuliwa na tumbo hadi umauti ulipomfika. Msiba upo nyumbani kwao Matumbi, Mwembeyanga Temeke Jijini Dar es Salaam huku mazishi yakitaraji kufanyika kesho Jumanne Februari 15, 2022 saa 7 mchana eneo la Kibada Wilayani Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Enzi za Uhai wake, Kondo alitumikia chama cha Soka Dar es Salaam kwa zaidi ya miaka tisa na kusifika kwa kuinua soka la vijana. Mungu ailaze roho ya Marehemu Kondo mahala pema peponi Amin.

