Ijumaa , 18th Mar , 2022

Mkurugenzi wa Sheria na Udhibiti wa kampuni ya uzalishaji wa bia za Serengeti (SBL), Lucia Minde, amesema kwamba kampuni hiyo imeanzisha kiwanda cha kutengeneza pombe kali ambacho wafanyakazi wake wote ni wanawake.

Lucia Minde, Mkurugenzi wa Sheria na Udhibiti kutoka Serengeti Breweries Limited

Minde ametoa kauli hiyo leo Machi 18, 2022, wakati akizungumza kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio na kusema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha wanaongeza asilimia kadhaa ya wanawake kwenye kampuni.

"Tuna kiwanda tulichoanzisha Julai mwaka jana, ambacho kinatengeneza pombe kali Moshi na wafanyakazi wote kwenye hicho kiwanda ni wanawake, yaani kuanzia pale getini walinzi ni wanawake," amesema Lucia.