
(Cristiano Ronaldo na Thiago Silva wakilalamika kwa muamuzi Mike Dean)
Manchester United na Chelsea sasa ndio timu zilitoka sare mara nyingi zaidi katika historia ya ligi kuu ya england EPL wakifikisha sare ya 55 katika michezo 172 waliokutana, na sare ya jana ni ya sare ya 26 katika dimba la Old Trafford. Nyota wa Manchester united Cristiano Ronaldo Do Santos amefunga magoli 8 kati ya magoli 9 ya mwisho yaliyofungwa na united.
(Kocha wa muda wa Manchester United Ralf Rangnik)
Kwa upande mwingine Shirikisho la soka nchini Austria linatarajia kumtangaza kocha wa muda wa manchester united Ralf Rangnick kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Austria saa chahche zijazo. Rangnick mwenye umri wa miaka 63 kwasasa ana makubaliano na manchester united kuwa mshauri wa masuala ya ufundi hadi mwaka 2024, na inatarajiwa kwamba Rangnick ataendelea na majukumu yake ya mshauri wa ufundi wa united wakati akiwa kocha wa taifa la Austria.