Jumatatu , 9th Mei , 2022

Kinda wa Hispania Carlos Alcaraz ameshinda ubingwa wa michuano ya wazi ya Tenisi ya Madrid (Madrid Open) jana usiku Mei 8, 2022. Baada ya kumfunga bingwa mtetezi wa michuano hiyo mjerumani Alexander Zverev kwenye mchezo wa fainali kwa seti 2 mfululizo 6-3 na 6-1.

Carlos Alcaraz Bingwa Madrid Open 2022

Alcaraz hili ni taji lake la pili kwenye michuano ya Tenisi (Tennis) ya Masters mwaka huu 2022, baada ya kuchukua ubingwa wa michuano ya Miami (Miami Open) mwezi Machi lakini pia hili ni taji lake la 4 mwaka huu.

Carlos Alcaraz mwenye umri wa miaka 19 katika safari yake ya bingwa huu katika hatua zilizopita aliwatoa magwiji Rafael Nadal bibgwa mara 21 wa Grand Slam na mshindi mara 5 wa Madrid Open katika ahatua ya robo fainali na alimtoa bingwa mara 20 wa Grand SlamNovak Djokovic hatua ya nusu fainali. Kwa sasa anashika nafasi ya 6 kwa ubora kwenye viwango vya ubora wa Tennis kwa wanaume.