Jeneza lililobeba mwili wa Padri Michael Samson
Viongozi wa dini na waumini, wakiongozwa na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mbeya ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Wakatoliki Tanzania (TEC) Gervas Nyaisonga, wameshiriki zoezi la kuaga mwili wa Padri huyo aliyeuawa Juni 11, 2022 na mwili wake kupatikana eneo la Sabasaba jijini Mbeya.