
Ndugu na majirani wa familia hiyo wanasema siku ya mwisho mtoto huyo alitoka nyumbani majira ya saa11 jioni kwa ajili ya kupeleka nguo za shule kwa fundi lakini tangu hapo hakuonekana mpaka mwili wake ulipookotwa ukiwa umetobolewa jicho na kusagwa unyayo.
Kutokana na matukio ya ukatili kwa Watoto kuongezeka mkoani humo Baadhi ya wanafunzi wenzie na marehemu wameiomba serikali kuwawekea mazingira rafiki kwa ajili ya usalama wao.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe anasema jeshi bado linaendelea na uchugnguzi juu ya tukio hilo linalohusisha imani za kishirikina.