
Akitoa taarifa za kufikishwa mahakamani watuhumiwa hao Kaimu Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya kuzuiya rushwa na uhujumu uchumi Zanzibar (ZAECA) Makame Khamis Hassan kwa kushirikiana na ofisi mkurugenzi wa mashtaka DPP amesema fedha hizo ni fedha za mradi wa uimarishaji wa mazingira ya kujifunzia wanafunzi Zanzibar (ZISP)
Aidha makame amesema mamlaka imewasilisha kwa DPP jumla ya majalada 12 yaayohusiana na tuhuma mbali mbali za rushwa na uhujumi uchumi kwa hatua zaidi