Ijumaa , 16th Sep , 2022

Mwanamke mmoja mwenye  umri wa miaka 22 nchini Iran amefariki dunia siku chache baada kuachiliwa na polisi ambao walimkamata kwa kosa la kutofunika kichwa chake.

 

  Mashuhuda wanasema kwamba mwanamke huyo aitwae Mahsa Amini alipigwa akiwa ndani ya gari la polisi wakati alipokamatwa huko mjini  Tehran jumanne ya wiki hii.

Polisi wamekana tuhuma hizo na kusema kwamba mwanamama huyo amefariki kwa matatizo ya moyo. 

Taarifa zinasema kwamba nchi hiyo imekua na mwendelezo wa report ya ukatili kwa wanawake katika wiki  za hivi karibuni. 

Familia ya marehemu Amini imesema kwamba ndugu yao alikua mzima wa afya na kwamba hakua natatizpo loloyte la moyo.