Mwanafunzi akipokea zawadi baada ya kufaulu
Akizungumza wakati wa utoaji tuzo hizo zilizotolewa na Umoja wa Wanakanyangereko -UMOKA, Mwenyekiti wa umoja huo Audax Ndyamukama amesema kuwa walifikia uamuzi huo baada ya kuona shule za kata hiyo hazifanyi vizuri katika mitihani ya kitaifa.
Aidha amefafanua kwamba wanafunzi walionufaika na tuzo hizo ni kutoka katika shule za msingi za Byeya, Nyakabanga, Nyakataare, Kabagara, Nyarubale na Ntoma, na mwalimu Evelina Leonard wa somo la Kiswahili kutoka katika shule ya msingi Nyakabanga.
"Tukaona tuanzishe programu ya kuamsha ari inayoitwa Umoka Academic Awards, ambayo itakuwa inatoa tuzo kwa wanafunzi na walimu waliofanya vizuri, pia na shule iliyofanya vizuri, tunaamini kupitia zawadi hizi wanafunzi na walimu wataongeza bidii katika masomo, ufundishaji na nidhamu, na katika vile vitu vyote ambavyo vinapelekea mtoto kufanya vizuri" amesema Ndyamukama.

