. Kimbunga Nanmadol tayari kimeshaua watu wawili mpaka sasa na kujeruhi watu takribani 90.
Kimbunga hicho kimepiga kisiwa cha Kyushu siku ya jana na mamlaka za hali ya hewan nchini humo zinasema kwamba kimbunga hicho kitaendelea katika visiwa vya Honshu ndani ya siku chache zijazo.
Makumi ya watu walitumia siku ya jana kujihifadhi kwenye makazi ya dharura ,huku nyumba takribani 350,000 zikikosa umeme.
Usafri na bisahara vimeathiriwa vibaya huku kukiwa na mafuriko na mmomonyoko wa udongo. Kimbunga Nanmadol kimeleta upepo wenye ksi ya kilomita 234 kwa saa huku baadhi ya maeneo yakipigwa na mvua zenye ujazo wa milimita kwa saa 24.

