
Romana Kimambo amesema wamekua wakipokea taarifa za walimu kuchukua mikopo kutoka taasisi binafsi za kifedha kwa masharti magumu ambayo huwalazimu kuacha kadi ya kutolea fedha benki (ATM) na namba za siri au hata vitu vya thamani kama dhamana hali inayowaweka katika wakati mgumu pindi unapofika muda wa marejesho.
Changamoto hiyo inayowakabili walimu ikamfikia mbunge wa jimbo la Kisarawe pia ni Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira Mh. Seleman Jafo ambae anakiri kuwepo kwa kadhia hiyo na hapa anatoa ushauri kwa walimu kote nchini kutumia muda wanaotoka kazini kujikita katika shughulisha mbalimbali za uzalishaji mali ili kujiongezea kipato.
Aidha waziri JAFO amewaasa walimu wazazi na walezi kuhakikisha wanasimama kidete ili kuwalinda watoto dhidi ya matukio ya ukatili yanayojitokeza katika maeneo mengi nchini.