Jumatano , 5th Oct , 2022

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro amesema ni vema vyuo vikuu vyote nchini vikazingatia ubora wa Kimataifa ili kutoa wahitimu wenye msaada kwa taifa na ulimwengu.

Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam

Dkt. Laurean Ndumbaro ambaye ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ametoa ushauri huo Oktoba 05 alipozungumza na wandishi wa habari alipohudhuria muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ndaki ya Sayansi za Jamii akiwa mgeni rasmi, na kwamba suala la ufundishaji pia liangaliwe kutokana na Maendeleo ya teknolojia ya mtandao.

"Kwakuwa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu vipo kuitumikia na kuisaidia jamii, ni vema vyuo vyote nchini vikatoa elimu kwa kuzingatia viwango vya kimataifa kwakuwa wataalam tunaowatoa wanatakiwa kuisaidia dunia na taifa pia. Kwahiyo lazima vyuo vihakikishe kwamba wataalam wetu wanakuwa na viwango vya kimataifa kwasababu ni mhimu kwa taifa na ulimwengu wote, siyo Tanzania tu. Lakini pia sasa hivi, kwasasa hivi kuna Maendeleo makubwa ya Internet kwenye ulimwengu, wanafunzi wanaweza kupata material kwenye mtandao. Hivyo basi, tuhakikishe kwamba tunaanagalia namna ya ufundishaji wetu uendane na mabadiliko ya teknolojia" - Dkt. Laurean Ndumbaro - Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

 Aidha, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. William Anangisye, akizungumzia namna chuo hicho kinavyoshiriki kuisaidia jamii kuleta usawa wa kijinsia, amesema kwa sasa wamefikia udahili wa 50/50 ili kuleta usawa wa wataalam, huku rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii akisema tafiti ni mhimu kwa maendeleo ya jamii.

"Wakati ndaki ya sayansi za jamii ikishiriki kwenye maadhisho haya, tayari ndaki hiyo inasherekea pia kufanikiwa kuleta usawa wa kijinsia na hadi sasa asilimia hamsini na moja ya Wanafunzi pale ni wakike. Hili linafanywa ili kuwa na uwiano wa uzalishaji wa wataalam kusudi jamii ipate wataalam hawa na kuhamasisha usawa pia kwenye jamii"- Prof. William Anangisye, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam.