
Bangi Marekani
Msamaha huo utawanufaisha raia takribani 6,500 wa nchi hiyo waliohukumiwa adhabu mbalimbali, baada ya kupatikana na makosa ya utumiaji wa bangi.
Rais Biden amesema msamaha huo utawarahisishia watu wengi nchini humo kupata ajira, makazi na elimu, ambapo awali walionekana hawastahili kutokana na kutiwa hatiani.
Wakati wa kampeni zake za uchaguzi, Joe Biden aliahidi kuhalalisha matumizi ya bangi pamoja na kutoa msamaha kwa wote waliohukumiwa kutokana na makosa ya matumizi ya bangi endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Taifa la Marekani.
Rais Joe Biden amesisitiza kuwa hatua ya kuwafunga watu gerezani baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya matumizi ya bangi imewaumiza watu wengi na kuwarudisha nyuma kimaendeleo, na kwamba jambo hilo kwa sasa halitaruhusiwa.